amekwama kufika
katika mkutano huo kutokana na kukosa usafiri kufuatia gari lake kuwepo
katika usimamizi wa mitihani ya Taifa kwa wanafunzi wa Darasa la Saba.
“Ndugu zangu
wananchi kwa niaba ya Mkurugenzi napenda kuwaomba radhi kwa kuchelewa
kufika hapa mgeni wetu sasa ni saa tano asubuhi ,ni kwamba mgeni wetu
hataweza kufika kutokana na kukosa usafiri wa kumleta hapa,gari lake liko
kwenye shughuli za Mitihani ya Darasa la saba”alisema Bulugu huku miguno na
maswali toka kwa wananchi vikitawala.
“Hivi Mtendaji huoni
kuwa huu ni uzembe wa makusudi,magari yote ya Halmashauri hayapo kweli? hata
gari lake liko kwenye mitihani?mbona hawa watu wanataka kuturudisha
tulikotoka? Sasa tunakuagiza Mtendaji ukamwambie Mkuu wa Wilaya kuwa agizo
lake limepuuzwa! kwa nini Mkurugenzi asitumie hata Hiece?” alihoji mmoja wa
wananchi waliokuwepo katika mkuitano huo.
Yaliyojiri baada ya Uchunguzi
Uchunguzi uliofanywa
kipindi hicho Tanzania Daima lilibaini kuwa, taarifa hizo hazikuwa za kweli
kwani Mkurugenzi huyo alikuwa safari ya kikazi Mjini Dodoma.
taarifa hiyo iliwakera
wananchi na kuahidi kugomea mikutano ijayo iwapo hawatapata maelezo ya
kutosha juu ya tukio hilo ambapo hadi leo hii wananchi hao hawajawahi
kusikilizwa kutokana na kwamba mkutano huo ulikuwa kama kiini macho kuficha tuhuma
zilizokuwepo kwa watumishi kipindi hicho.
Mwandishi wa
Tanzania Daima alimtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi ili kutolea ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa
na Afisa Mtendaji huyo ambapo Mkurugenzi alisema kuwa hazina ukweli.
“Mimi kwa sasa niko
Mbeya,nimeshtushwa sana na taarifa hizo mimi nikose usafiri si ningeenda na
pikipiki? Sisi kazi yetu ni moja tu nayo ni kuwatumikia wananchi na si
vinginevyo sijui Mtendaji huyo kapata wapi maelekezo hayo ngoja
nifuatilie”alisema Mwaiteleke.
Wakizungumza na
Tanzania Daima kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema kuwa wamekwazwa na
kitendo cha Mkurugenzi kushindwa kufika kijijini jambo walilosema bila
kumung’unya maneno kwamba ni uzembe.
Akiweka wazi siri
zilizokuwa zimefichika katika maandalizi ya taarifa za uongo zilizotolewa na
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Sanjo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyasubi
Meni Lutandula aliliambia Tanzania Daima kuwa kuna udanganyifu mkubwa
katika ujenzi wa tenki la maji katika kijiji cha Sanjo ambapo walibaini
matumizi mabaya ya fedha za wananchi kiasi cha shilingi milioni 20,828,502;60 katika
ujenzi wa mradi wa maji.
“Inasikitisha kuna
ujenzi wa shule ambayo hata hivyo ilikuwa haijaanza kufanya kazi lakini
tayari vyumba vimechakaa kutokana na kujengwa chini ya kiwango wananchi kulazimishwa
kuchangia shilingi 6500 kila familia kwa ajiri ya ukarabati wa vyumba
hivyo”.alisema Lutandula.
Mwenyekiti wa Kijiji
cha Sanjo Bukali John alipotakiwa kutolea ufafanuzi sakata la ujenzi wa
madarasa chini ya kiwango alisema alikiri na kumuonya mwandishi asiripoti
taarifa hizo.
“Nisingependa uendelee
kufuatilia jambo hilo kwa kuwa wananchi tayari tumeshawashawishi
wananchi na wamekubali kuchangia fedha kwa ajiri ya kurekebisha vyumba hivyo ni
kweli kuna mapungufu yaliyojitokeza katika ujenzi wa vyumba hivyo lakini
sitaki ufuatilie suala hilo maana tayari tumeshafanya vikao na wananchi na tumekubaliana
wachangie fedha kiasi cha shilingi 6500 kila familia ili tuweze kukarabati
vyumba hivyo” alisema Bukali.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda alipotafutwa kuzungumzia kama alitoa agizo
kwa Mkurugenzi ambapo alisema kuwa hana taarifa zozote juu ya agizo hilo na
kwamba yeye hajawahi kufanya ziara katika kijiji cha Sanjo.
“Mimi sijawahi
kufanya ziara yoyote katika kijiji hicho isipokuwa nilishiriki kikao cha Kamati
ya Maendeleo ya Kata ya Fela hivyo sijui Afisa Mtendaji huyo alitoa wapi
maelekezo hayo nitafuatilia kujua zaidi juu ya jambo hilo”alisema Sweda.
Baraza la Madiwani kuwapa Siku 30 kwa
watendaji
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya
ya Misungwi, limewapa muda wa siku 30 watendaji kushughulikia suala la
makusanyo ya mapato ya ndani na utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji
cha Fela uliokwama tangu 2013.
Azimio hilo lilipitishwa na baraza hilo wakati wa kikao kilichofanyika mjini Misungwi juzi, baada ya kubainika kuwa hadi Desemba 2017 halmashauri hiyo imekusanya Sh734.9 milioni pekee kati ya malengo ya kukusanya Sh2.06 bilioni. Katika Baraza hilo Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga aliwacharukia watendaji na kuwataka watoe maelezo juu ya kusuasua kwa ukusanyaji mapato, hali inayokwamisha utekelezaji wa miradi. Akitolea mfano wa kusuasua alisema kuwa katika mwalo huko Mbarika vitabu vya halmashauri vinaonyesha hakuna mapato yanayokusanywa, lakini hivi karibuni kamati ya uchumi na mipango ilipotembelea eneo hilo ilifanikiwa kukusanya Sh15,000 kwa muda mfupi, hali inayodhihirisha udhaifu katika ukusanyaji wa mapato. Kuhusu mradi wa maji wa Fella ambao utekelezaji wake ulianza Juni 2013 na kutakiwa kukamilika Desemba mwaka huo, baraza limempa siku 30 mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke kuhakikisha unakamilika na kutoa maji au uwekwe chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Mradi huo ambao tayari umegharimu zaidi ya Sh644 milioni, unatarajiwa kunufaisha wakazi 6,473 wa vijiji vya Fella, Ngeleka na Bujingwa. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, mhandisi wa maji wa halmashauri hiyo, Ali Mruma alisema tayari maji yameanza kutoka na zinahitajika zaidi ya Sh3.8 milioni kununulia mashine ya kuyasukuma ili kuongeza usambazaji wa huduma kwa wananchi. Diwani wa viti maalum, Christina Nyanda alisema maji hayo kata ya Mamaye yanatoka kwa kusuasua na kutaka wataalamu kutoa maelezo sahihi. Mkandarasi wa kampuni ya COWI Tanzania Ltd inayotekeleza mradi huo, Ernest Tinka alikiri kuwapo upungufu na kuahidi kurekebishwa.
Siri
zilizofichika nyuma ya miradi Misungwi.
1.
Kuna maslahi binafsi katika utekelezaji
wa Miradi mbalimbali Wilayani Misungwi kutokana na baadhi ya viongozi wa
Serikali na kisiasa kudaiwa kuwa ndiyo wamiliki wa makampuni yanayotekeleza
miradi hiyo ambapo kwa haya aliyokutana nayo Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Suluhisho
kuinusuru Miradi ya maendeleo dhidi ya Mchwa.
inatakiwa
kuunda Tume Maalumu kwa ajiri ya kuchunguza ufujaji wa mali za Umma lakini
pia watumishi wa Wilaya ya Misungwi wahamishwe kutokana na Mtandao wao unaokwamisha
kujulikana kwa uozo kupitia kwa Kaimu Afisa Habari wa Wilaya ya Misungwi
Thomas Lutego ambaye hata akiwa na shughuli hubagua Waandishi wa Habari kwa
lengo la kuficha maovu hayo.
|
|
Monday, February 19, 2018
Hongera Waziri Mkuu kufanya ziara Mwanza
Posted on 11:09 PM by sndffoundation
Antony Sollo Misungwi
Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Kassim Majaliwa Jijini Mwanza imekuwa ya mafanikio,hii ni baada ya
kubaini mambo uozo lakini haya ni kwa uchache kutokana na siri kubwa iliyofichika
kutokana uozo mwingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya
Misungwi Mkoani Mwanza.
Historia ya kuwepo kwa Uozo Misungwi.
Wilaya ya Misungwi ni moja kati ya Wilaya
kongwe nchini ambazo zimekuwa zikiongoza kwa kupata hati chafu na imekuwa
bahati kwa Mawaziri Wakuu wa awamu ya Nne na ya tano ambao wote wamebahatika
kukumbana na uozo jambo lililopelekea kuwatumbua watumishi wachache wa
Halmashauri hiyo huku vinara wakiachwa kutokana na kuwepo kwa mnyororo mkubwa
ambao umetengenezwa maalumu kwa ajili ya upigaji dili.
Katika ziara yake hivi karibuni,Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Khassim Majaliwa amemsimamisha
kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Alphonce
Sebukoto, na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.
Waziri Mkuu alifikia hatua hiyo baada
Mwanasheria huyo kuonekana kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni
pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia hasara ya
sh. milioni 279.
Majaliwa alimsimamisha kazi Sebukoto 19februari
mwaka huu wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo akiwa
katika ziara ya siku tano ya kikazi mkoani Mwanza ambapo waziri Mkuu alisema.
“Mwanasheria utasimama kazi kuanzia
leo na tuhuma zako zitachunguzwa kikamilifu na vyombo husika na uchunguzi
ukibaini kama huna kosa utarudi kazini. hatutakuonea lakini hatuwezi
kukuvumilia kwa utaratibu huo ulioufanya,” alisema Majaliwa.
Imeelezwa kuwa Novemba 2017 wakati
alipokuwa anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo ya
sh. milioni 279 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo, Antony Bahebe.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mkuu Bahebe
aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya
ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi ya
Seekevim ambapo alisema mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa
ukamilike 2015,ambapo Mwanasheria huyo
aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa
imekwisha tangu Desemba 2015.
“Mwanasheria amemlipa Mwenyekiti wa
Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri baada ya kuifikisha Halmashauri
yake Mahakamani. Amemlipa fedha wakati kazi yenyewe ilikuwa haijaisha na
aliharakisha malipo hayo kipindi ambacho Mkurugenzi hayupo, ”alisema Majaliwa huku akiwakumbusha watumishi wa umma
kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Akifafanua Majaliwa alisema fedha
alizolipwa Bahebe zingeweza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya
maendeleo katika halmashauri hiyo.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu alifungua mabweni ya watoto wenye mahitaji maalumu
katika shule ya msingi ya Mitindo iliyoko wilayani Misungwi na pamoja na kukagua
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Ukiacha na kipande hicho cha uozo
uliofichwa,Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imekuwa na historia mbaya kwa
watendaji wa Wilaya hiyo kutafuna fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo
ambapo baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo wamekuwa wakibuni mbinu
mbalimbali kuwahadaa wananchi.
Mwaka 2016 Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Sanjo Charles Bulugu,alimchongea
kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Eliud Mwaiteleke kwa
kutoa taarifa za uongo katika mkutano wa Serikali ya Kijiji cha Sanjo
akisema kuwa,Mkurugenzi huyo alishindwa kufika katika mkutano wa kijijinihicho
kwa kukosa gari la kumpeleka kusikiliza kero za wananchi hao.
Katika mkutano huo Bulugu
alidai kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi alitoa agizo akimtaka Mkurugenzi kufika
katika kijiji hicho kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wananchi wa Kijiji cha
Sanjo kwa kuuomba Uongozi wa Wilaya ya Misungwi ufike hapo kusikiliza kero zao.
Katika taarifa hiyo iliyotengenezwa ili kuwahadaa wananchi wa
Kijiji cha Sanjo Bulugu alimsingizia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Eliud
Mwaiteleke kuwa eti
Wednesday, February 14, 2018
Bundi atua Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Posted on 1:37 PM by sndffoundation
Na Antony Sollo Ushetu.
14feb 2018
MGOGORO mkubwa umeibuka baina ya Emmanuel Makashi ambaye
ni Diwani wa Kata na Christopher Rwagasanga Lyogelo ambaye ni Afisa Mtendaji wa
Kata ya Sabasabini iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoni Shinyanga,hali
iliyopelekea diwani huyo kuangua kilio katika kikao cha baraza la Madiwani wa
Halmashauri hiyo akimtuhumu Afisa mtendaji huyokuhujumu shughuli za maendeleo
ya Kata hiyo.
Akiwasilisha malalamiko yake mbele ya Madiwani hao kilichofanyika
Februali 14 mwaka huu huko Ushetu Makashi lisema kuwa Afisa Mtendaji huyo
amekuwa akibeza kila kitu kinachofanywa na Diwani huyo.
“Mheshimiwa mwenyekiti Afisa Mtendaji huyo amekuwa akichonganisha
na wananchi huku akisema kwamba mimi sijasoma,na kuwaambia kuwa yeyendiye
anafaa kuwa kiongozi wao akidai kuwa anashahada ya elimu ya juu na kuwaambia kwamba
mimi sina uwezo wa kuwaletea maendeleo amekuwa akiwashawishi watendaji wa vijiji
kutojishughulisha katika masuala mbalimbali ikiwemo uchangiaji wa shughuli za maendeleo”alisema
Makashi.
Kutokana na uchungu aliokuwa nao Makashi aliangua
kilio mbele ya viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao cha baraza la Madiwani
wa Halmashauri hiyo kilichoketi kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ya
maendeleo ikiwamo miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Ushetu.
Baraza hilo lilihudhuriwa na viongozi mbambli mbali wa
Chama na serikali akiwemo mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa
pamoja na katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya ambapo Diwani huyo
aliamua Mtendaji huyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga huku akisema.
“Ndugu mwenyekiti kuna tatizo la kiutendaji katika Kata
yangu ya Sabasabini kwamba, Afisa Mtendaji wa Kata amekuwa kikwazo kikubwa cha
maendeleo kwa wananchi wangu, tangu aanze kazi kwenye Kata yangu mwaka 2016
hakuna maendeleo yoyote kwani amekuwa akiwagomesha wananchi kuchangia shughuli
za maendeleo,” alilalamika Makashi.
Katika jitihada za kutatua mgogoro huo Makashi
alimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Matomola Michael kufika
katika Kata hiyo ili kuwapatanisha waendelee kuwatumikia wananchi huku akisema
tangu kuanza kwa figisu figisu za Afisa Mtendaji huyo hadi sasa hakuna kitu kinachofanyika
kutokana na mgogoro huo.
“Mheshimiwa mwenyekiti kibaya zaidi Afisa Mtendaji huyo
amekuwa akiwashawishi na watendaji wengine wa vijiji wasinipe ushirikiano
katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wananchi kwa madai kwamba yeye
ndiye kiongozi sahihi kutokana na kwamba ana nashahada ya elimu ya juu,kwa
kweli nakuomba Mkurugenzi aunde tume ya uchunguzi dhidi yake,kama hutafanya
hivyo tubadilishane ofisi wewe uwe diwani na mimi nikae kwenye kiti chako cha
ukurugenzi ili na wewe uone vitendo ninavyofanyiwa na Mtendaji huyo,” alisema
Makashi kwa uchungu.
Makashi alisema kuwa,kabla ya ujio wa Afisa Mtendaji huyo
katika Kata ya sabasabini, kulikuwa na mahusiano mazuri na wananchi kutokana na ushirikiano mzuri kati
yake na kaimu afisa mtendaji aliyekuwapo kipindi cha 2013 /2015 kwa kufanikisha
kutimiza agizo la Rais Magufuli juu ya kutengeneza Madawati mashuleni ambapo
walifanikisha kuchonga madawati 74 yaliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 8.8
Makashi alisema kuwa katika kipindi hicho alijitolea katika
ujenzi wa matundu ya choo cha shule kwa kuchangia kiasi cha shilingi 150,000 na
kuongeza kuwa kiasi cha shilingi milioni 5.3 kilitumika kujenga nyumba ya
mganga katika Zahanati ya Kata huku nguvu ya wananchi ni shilingi milioni
1.2.
Makashi alibainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2017
alifanikisha kujenga barabara ya Sabasabini kwenda Iponyang’holo kiwango cha
changarawe yenye urefu wa kilometa 9 kwa gharama ya shilingi milioni 2.5 kwa
ushirikiano na diwani wake wa viti maalum Felista Nyerere ambaye alichanga
shilingi 300,000 kati ya fedha hizo,ambapo alidai kuwa tangu mtendaji huyo
aanze kazi shughuli za maendeleo zimesimama kutokana na mgogoro wao.
“Mtendaji huyo alianza kazi katika kata hii tangu
mwaka 2016, na alinikuta nikiwa vizuri na wananchi wangu lakini tangu
aanze kazi nimeshindwa kumuelewa labda anaitaka hii Kata!, maana kinachofanywa
na Mtendaji huyu ni uvunjaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ninaona
Mtendaji huyu anapingana na kasi ya Mheshimiwa Rais kwa kuamua kukwamisha shughuli
za maendeleo kwa makusudi,mimi naomba Mkurugenzi aunde hiyo Tume ili kuweza
kutatua mgogoro huu vinginevyo Kata hii haitaweza kupata maendeleo”alisema
Makashi.
Akichangia hoja hiyo Diwani wa Kata ya Bulungwa Joseph
Masaluta alilieleza baraza hilo kuwa wote wawili kwa maana ya Diwani pamoja na
afisa mtendaji huyo wa Kata wapelekwe kwenye kamati ya maadili kwa lengo la
kuhojiwa kwa kina ili kubaini chanzo cha mgogoro wao na kuongeza kuwa wawili
hao wamekutana wote ni jeuri.
Katika majibu yake kwa diwani huyo Makamu mwenyekiti
wa baraza hilo Gagi Lala ambaye ndiye alikuwa akiongoza baraza hilo alisema,
“Mkurugenzi haiwezekani mtu alalamike kiasi hiki tena
hadharani inaonekana kuna tatizo linalopaswa kushughulikiwa, pamoja na kwamba kanuni
za baraza haziruhusu kuingiza taarifa zilizo nje ya shughuli za baraza ,
mheshimiwa diwani ujumbe umefika kuwa mtulivu tutalishughulikia suala hili,”
alisema Lala.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Benjamin Onesmo ambaye pia ni afisa maendeleo
ya jamii katika Halmashauri hiyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo ofisi yake
imelichukua suala hilo na italitafutia ufumbuzi wa haraka.
“Mheshimiwa Mwenyekiti ofisi yangu inalibeba suala
hilo na litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa Haraka,” alisema Onesmo”.
MWISHO.
Sunday, February 11, 2018
Afisa biashara Manispaa ya Ubungo awaliza mamilioni wafanyabiashara .
Posted on 1:09 AM by sndffoundation
Na
Antony Sollo Ubungo.
AFISA
biashara wa Manispaa hiyo Geofry Mbwama anatuhumiwa kujipatia mamilioni ya
fedha toka kwa wafanyabiashara wenye maduka pamoja na wajasiriamali katika
manispaa hiyo baada ya kuingia kila duka akiomba Leseni ya biashara akiwa na
Dereva wa Manispaa hiyo na kufanikiwa kujipatia kiasi kikubwa cha fedha
akitumia nyaraka bandia za Serikali Tanzania Daima libaini.
Tukio
hilo lilitokea desemba 13 mwaka jana katika Mtaa wa Mbezi Luis Manispaa ya
Ubungo Jijini Dar Es Salaam ambapo Mbwama akiwa na gari la Manispa hiyo
aliingia katika maduka na vibanda vya wafanyabiashara wadogo mafundi pikipiki
hata wanaofanyia shughuli zao nje huku akihoji kama wana Leseni za biashara na
pale ambapo alikuta hawana kwa sababu mbalimbali alifunga biashara na makufuli
yake na baadaye aliandika nyaraka inayodaiwa kuwa ni feki na kuwapiga faini
kati ya 321,000.
Akithibitisha
kufanyiwa vitendo hivyo mmoja wa wajasiriamali (Fundi pikipiki) eneo la Mbezi
makabe road Rahesh Shaban ambaye anajishughulisha na ufundi wa pikipiki alisema
alilazimishwa kufunga shughuli zake baada ya kubainika kuwa hakuwa na leseni ya
kufanya kazi ya ufundi licha ya
kujitetea kuwa alikuwa ameenda katika mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya
kupatiwa namba ya utambulisho wa mlipa Kodi ( TIN Number) lakini Afisabiashara huyo
alimwandikia faini ya shilingi 321,000 na kumwamuru afunge shughuli zake.
“Mimi
na wenzangu hapa tumemweleza kuwa tunazo baadhi ya nyaraka na kwamba tayari
tulikuwa tumeshaanza mchakato wa kupatiwa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(
TIN Number) lakini hakutuelewa na matokeo yake aliandika faini katika nyaraka
ambazo tunahisi ni feki kwa kuwa nyaraka yoyote ya Serikali huwa haiandikwi
kitu chochote au namba ya mtu binafsi ambapo hata hivyo aliomba fedha kiasi
kati ya 20,000, mpaka 60,000 tukampatia na hakutoa risiti yoyote”alisema
Shabani.
Kwa
kuwa Shaban aliona kuwa mahala pale ndipo anapopata riziki kwa ajili ya
mahitaji ya familia yake,aliomba asamehewe lakini kilichoshangaza aliombwa
shilingi 20,000 na Mbwama lakini hakupatiwa risiti jambo ambalo pia
lilithibitishwa na wafanyabiashara wa duka la madawa yaliyoko jirani na Shabani
ambao nao walitoa fedha kiasi cha shilingi 60,000 kila mmoja kutokana na
kutishiwa kufungiwa maduka yao ambapo fedha hizo zilikabidhiwa kwa dereva wa
Manispaa ambaye naye alikuwa akiwakaripia wafanyabiashara na kutoa vitisho vya
kuwafungia biashara zao.
Tanzania
Daima lilifuatilia nyendo za Mbwama na kukutana na malalamiko lukuki kwamba
wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mtaa wa Mbezi walio wengi walikuwa
wameshachukuliwa fedha zao kutokana na tishio la kufungiwa biashara zao na
Afisa biashara huyo akishirikiana na dereva wake.
Mwandishi
wa gazeti la Tanzania Daima alimtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambapo
hata hivyo juhudi za kumpata Mkurugenzi huyo ziligonga mwamba kutokana na
mwingiliano wa majukumu ambapo lilikutana na Katibu Tawala James Mkumbo ambaye
baada ya kupatiwa taarifa juu ya kilichofanywa na watumishi hao dhidi ya
wafanyabiashara nawajasiriamali na kuahidi kuzifanyia kazi tuhuma hizo ambapo
tangu 13 desemba hadi leo hakuna taarifa zozote.
Mara
kadhaa Mkumbo amekuwa akitakiwa kutolea ufafanuzi wa tatizo hilo lakini amekuwa
akidai kuwa alikabidhi watu kufanyia kazi tuhuma hizo
“Kwa
sasa niko Mwanza lakini kuna watu niliwapa jukumu la kushughulikia suala hilo
lakini pia sisi hatufanyi kazi kwa pressure za waandishi wa Habari kwa sababu
wanataka habari tukikamilisha utaratibu wetu tutafanya kinachostahili ”alijibu Mkumbo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi.
Kinachoshangaza
hapa ni kwamba hakuna taarifa zozote kuhusu ufuatiliaji wa tuhuma hizi pamoja
na Katibu Tawala huyo kupelekewa Ofisini tuhuma zinazowakabili Afisa biashara
wa Manispaa pamoja na dereva wa Manispaa ya Ubungo kwa takribani miezi miwili
sasa jambo linalozua sintofahamu juu ya uadilifu wa watumishi hao
Wananchi
waliozungumza na gazeti hili wameiomba Serikali kuwachunguza baadhi ya
wafanyakazi wake hasa waliotumbuliwa kwa kuwa sasa wengi wako mtaani hawana
kazi na wamegeuka Matapeli wanaotumia mbinu walizokuwa wamezizoea wakiwa kazini
kutafuta fedha kwa njia za vitisho na inasemekana Mbwama na dereva wa Manispaa
ya Ubungo kwa pamoja wamejipatia mamilioni kwa njia hiyo.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo John Kayombo hakuwez kupatikana mara moja kuzungumzia
tuhuma hizo ambapo juhudi za kumtafuta atolee ufafanuzi wa hatua gani
zimechukuliwa dhidi ya tuhuma kwa watumishi hao kwa kukiuka maadili ya Utumishi
wa Umma
MWISHO.
Friday, February 9, 2018
Wanaume waaswa kutojimilikisha maeneo ya familia
Posted on 10:41 AM by sndffoundation
Na Antony Sollo
Februari 9,2018.
WANAUME katika halmashauri ya mji wa Kahama
Mkoani Shinyanga wametakiwa kuachana na dhana ya kujimilikisha hati
miliki za viwanja vyao, ili kutoa kipaumbele kwa akinamama ili nao
waweze kumiliki ardhi hali ambayo itaepusha migogoro katika
familia.
Akizungumza kabla ya kutambulisha mradi wa upimaji wa
viwanja 4,000 katika kata ya Mhongolo afisa ardhi wa halmashauri ya
mji wa Kahama Mashiri Magasa alisema kuwa wanaume
wilayani Kahama wamekuwa na tabia ya kujimilikisha maeneo yote yenye hati
miliki jambo ambalo siyo haki na kwamba hali kama hiyo pindi mwanaume
anapofariki dunia humwacha mwanamke katika wakati mgumu.
Magasa aliyasema hayo februari 8 mwaka huu wakati
akizungumza na wananchi wa vitongoji vya sofi, bomani na Nyamhela vilivyoko katika
Mtaa wa Mhongolo ambapo aliwaasa wanaume kuachana na dhana ya kujimilikisha
maeneo ya familia kwani hali hiyo ndiyo chanzo cha mifarakano katika familia
pindi baba wa familia anapoamua kuchukua hati hizo na kuomba mkopo katika
taasisi za fedha na kushindwa kurejesha.
“Ifike wakati wanaume muwape fursa ya kumiliki ardhi wanawake
kwani kufanya hivyo kunatoa usawa katika familia lakini pia kuna wakati mmoja
wa familia hiyo akifariki hasa baba mwanamke hawezi kuhangaika kutokana kuwa
tayari anakuwa ana mali halisi inayomfanya aendeleze familia, wanaume wakiachana
na mfumo dume mwanamke akashirikishwa ipasavyo katika umiliki huo
hakutakuwepo na migogoro baina yao,” Alisema Magasa.
Katika hatua nyingine Afisa ardhi aliwataka wakazi wa
mji wa Kahama kuhakikisha wanapima viwanja vyao kabla ya kufanya ujenzi au
shughuli zozote za kimaendeleo na upimaji huo uende sambamba na utafutaji wa
hati miliki ili kupunguza migogoro isiyokuwa na tija kwa jamii na kuwafanya
waweze kukopesheka kirahisi katika taasisi za fedha.
“Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi na mpango miji hakuna
mwananchi yoyote hapa nchini anayeruhusiwa kufanya ujenzi wowote wa nyumba za
makazi katika kiwanja chake bila ya kupimwa au kujenga nyumba bila ya kufuata
ramani za mpango miji tukikuta unajenga kwenye eneo bila kibali tunasitisha
ujenzi na kukupiga faini” alisema Magasa.
Kwa mujibu wa mpima ardhi kutoka kampuni
ya Total Geo survey Co.Ltd
Emmanuel William ambaye anayeshughulikia upimaji wa
viwanja katika kata hiyo alisema kuwa wananchi wanatakiwa
kuchangia gharama za upimaji ili kazi iweze kuendelea na kwamba
mpaka sasa viwanja 4,000 vimepimwa na viwanja 1000 vimepitishwa
na wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa
ajili ya kuwatafutia hati miliki wananchi.
Akizungumzia zoezi hilo William alisema kuwa lengo ni
kupima viwanja 12,000 katika Kata hiyo na kuwataka wananchi kuongeza kasi ya
kuchangia gharama ya upimaji ambayo ni shilingi elfu tisini 90,000 na kwamba
gharama hiyo ni ndogo ukilinganisha na bei elekezi ya serikali ya kuanzia ambayo
inaanzia shilingi laki tatu, 3,000,000. Kwa kila kiwanja.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mhongolo
Denis Diocles alisema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kupima
viwanja elfu 12, lakini viwanja vilivyofikiwa ni 4021, vilivyopewa namba ni
1335, ambavyo havijapewa namba ni 2686 na kutaja mradi wote unagharimu kiasi
cha shilingi milioni 361 kati ya hivyo vilivyolipiwa ni 1192 na ambavyo
havijalipiwa ni 2828.
Akizungumza katika zoezi la kutamburisha mradi huo Mwenyekiti
wa mtaa wa Mhongolo Emmanuel Nangale alisema kuwa kukusanya shilingi milioni
361 kwa wakazi hao siyo kazi ndogo na kudai kuwa kiasi kilichokusanywa
hadi sasa kinapswa kupongezwa licha ya watu kutohamasika kikamilifu na kwamba
katika halmashauri hiyo ni Mtaa wa Mhongolo pekee umejitutumua katika zoezi
hilo.
Mwisho.
Monday, November 6, 2017
Waziri Mpina atoa siku mbili Ng’ombe 640 zirejeshwe kwa Wafugaji
Posted on 12:46 PM by sndffoundation
Na
Antony Sollo - Katavi
October
5 2017
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameupa
siku mbili Uongozi wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa – Lukwati kurejesha
mara moja ng’ombe wapatao 640 waliosalia ambao ni mali ya wafujaji
watatu kwa kuwa walikuwa wanashikiliwa kwa muda wa mwaka mmoja kinyume cha Sheria .
Waziri Mpina alitoa agizo hilo Oktoba 5 mwaka
huu wakati alipotembelea hifadhi hiyo iliyopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani
Mlele Mkoa wa Katavi kwa lengo la kutatua mgogoro wa muda mrefu
baina ya wafugaji hao watatu na uongozi wa hifadhi hiyo .
Imeelezwa
kuwa ng’ombe wapatao 692 ambao ni miongoni 1,332
walioshikiliwa na kuzuiliwa katika Hifadhi ya Pori la Akiba la Rukwa –
Lukwati kwa zaidi ya mwaka mmoja wamekufa kwa kukosa matunzo bora.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mpina alionyesha kushutushwa na taarifa iliyosomwa kwake na
Meneja wa Hifadhi hiyo,Paschal Mhina kuwa ng’ombe wapatao 1,332
waliovamia hifadhi walikamatwa na kushikiliwa kwa mwaka mmoja
na miezi tisa ambapo ng’ombe wapatao 692 wameshakufa na waliobakia ni 640
tu .
Mpina aliuagiza
uongozi wa Serikali ya mkoa wa Katavi kuhakikisha unahakiki mifugo
hiyo na kuwakabidhi wenye mali na kwamba wale wote watakaobainika
kusababisha vifo vya ng’ombe hao waliokufa kwa uzembe wachukuliwe hatua
kali za kinidhamu na za kijinai .
“
Hakukuwa na sababu yoyote ile ya msingi ya
kuendelea kuishilikia mifugo hiyo baada ya wenye
mali hiyo kufungua mashitaka mahakamani ambapo katika
kesi ya awali watuhumiwa watatu ambao ndiyo wenye mali hiyo walifungua
mashataka katika Mahakama ya Wilaya
ya Mpanda ambapo mahakama hiyo iliamuru
itaifishwe na iwe mali ya Serikali”
alieleza .
Waziri
huyo alimtaka Meneja wa pori
la Akiba amwonyeshe hati
yoyote inayowapa mamlaka ya kuendelea
kuwashikilia ngombe hao wakati wafugaji walikuwa wanatuhumiwa
walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga kupinga
kutaifishiwa ngombe zao lakini
hakuweza kufanya hivyo.
Hata
hivyo imebainika kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ilitengua
hukumu iliyotolewa na Mahama ya Wilaya ya Mpanda na
kuamuru wafugaji hao watatu warejeshewe mifugo yao na faini
ya Sh 500,000/- walizotozwa .
Wafugaji
hao watatu ni pamoja na Shigela Mayunga , Charles Mtokambali na Keleja
Makuja .
“Nimesikitishwa sana
na kitendo cha Uongozi wa hifadhi ya Pori la akiba la Rukwa –
Lukwati kwa kuendelea kuishikilia mifugo hiyo ambapo idadi kubwa ya
mifugo hiyo imekufa kwa magonjwa nataka kujua kwa nini
mifugo hiyo iliendelea kushikiliwa ndani ya hifadhi hiyo huku
eneo hilo likiwa limetengwa maalumu kwa ajili ya wanyamapori na sio
ng’ombe” alihoji Mpina huku akionyesha hisia kali kufuatia ukatili
uliofanywa.
Kwa
upande wake Meneja wa Pori la Akiba la Rukwa Rukwati
Mhina alieleza kuwa mifugo hiyo ilendelea kushikiliwa
kwa kile alichodai kuwa baada ya
uongozi wa hifadhi hiyo kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu
Kanda ya Sumbawanga.
Akijitetea
Mhina alisema kuwa ungozi wa hifadhi hiyo ulipewa maelekezo na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa waendelee kuitunza mifugo hiyo
kama sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo ..
Kwa
upande wake , Katibu Mkuu wa Chama cha
Wafugaji Tanzania Makoye Nkonosinema alisema kuwa mifugo
iliyokufa ikiwa mikononi mwa uongozi wa hifadhi hiyo
wataendelea kuidai
Aidha
alitaka kupewa maelezo ya kina katika kipindi hicho chote ambacho ng’ombe
hao walikuwa wameshikiliwa ni ndama wangapi waliozaliwa .
Naye Ofisa
Utafiti wa Magonjwa ya Mifugo wa Mikoa wa
Katavi na Rukwa , Protus Reshola alisema kuwa idadi hiyo ya ng’ombe
iliyokufa ni kubwa sana kwamba imesababishwa na dosari kadhaa
ikiwemo waliokuwa wakiwachunga walikuwa sio wafugaji .
Aliongeza
kuwa kutopatiwa matibabu stahiki na kutokuwepo na josho kwenye hifadhi
hiyo kumesababisha ng’ombe hao kufa kutokana na ugonjwa wa homa ya
mapafu .
Mwisho
Saturday, September 9, 2017
Wananchi Maganzo waiponda Kamati ya Ndugai.
Posted on 4:18 AM by sndffoundation
· Wasema iliacha
kuangalia matatizo ya wananchi
· Ilienda kwa ajili
ya kuangalia madini pekee.
· Wasema huo si
uzalendo,Utaifa.
· Kamati hiyo
haikufanyia kazi Mgodi wa Elhilal ulioko hapo
Na Antony Sollo Shinyanga.
09.09.2017
WANANCHI wa Mji mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu Mkoa wa
Shinyanga wametoa maoni yao kuhusu ripoti iliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli huku wakiiponda Kamati
iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
wakisema Kamati hiyo ina mapungufu makubwa Tanzania Daima limeelezwa.
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wahanga wa mgodi huo George
Joseph ambaye alipigwa risasi na walinzi wa mgodi huo ameilalamikia Kamati hiyo
kwa kushindwa kuangalia maisha ya Raia na badala yake Kamati hiyo imedaiwa
kujikita zaidi kuangalia wizi wa Madini ya Almasi katika Mgodi mmoja huku Mgodi
unaomilikiwa na Phantom ambaye anamiliki Kampuni ijulikanayo kama Elhilal
Mining ukiachwa bila kuchukuliwa taarifa zake yakiwemo mauaji ya wananchi
wakazi wa Maganzo.
“ Ripoti ya Kamati hii ina mapungufu makubwa sana kwani ujio
wake haukulenga kukutana na wahanga na pia ilipata makengeza kwa kushindwa
kuuona mgodi wa Elhilal Mining unomilikiwa na Pantom ambapo Kamati hiyo
imekutana na watu ambao taarifa zao zimejikita kwenye madini pekee lakini
haikukumbuka kama kuna matukio makubwa ya Mauaji, unyanyasaji wa raia kama
ilivyokuwa katika Kamati iliyoundwa kuchunguza zoezi la Operation Tokomeza
ambapo Kamati hiyo ilizama zaidi katika masuala ya Haki za Binadamu kujua
matatizo yiyowapata raia”alisema George.
George ameeleza kusikitishwa kwake na ubaguzi uliofanywa na Mkuu
wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba kwa kuwazuia waathirika waliopigwa
risasi na walinzi wa Mgodi wa Mwadui kuingia katika kikao cha Kamati hiyo ili
kueleza hali halisi na yanayojili kila siku katika Mgodi wa Mwadui na kwamba
eneo la Mgodi wa Mwadui halimilikiwi na WDL pekee bali kuna mwekezaji mwingine
ambaye amekuwa tishio kwa usalama wa raia kutokana na kuua vijana wengi na haku
akilindwa na viongozi wa Serikali na hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa
dhidi yake.
“Mwekezaji huyu ameua watu wengi na viongozi wa Jeshi la Polisi
na Madaktari waliokuwepo kipindi cha awamu ya Nne walikuwa na mnyororo mkubwa
wa rushwa ambapo vijana wengi waliuawa na kupelekwa gerezani huku mmiliki wa
Kampuni ya Elhilal akishinikiza vijana wanaokamatwa kupelekwa gerezani na
kuwekwa mahabusu kwa lengo la kutukomoa,Phantom amediliki kunyang’anya maeneo
ya watu lakini Serikali ilikuwa imewekwa mfukoni hebu tumuombe Mh Rais aje
tumweleze mateso tuliyo nayo sisi wananchi wa Maganzo”alisema George.
Kwa mujibu wa George Joseph ambaye ni mmoja wa waathirika
kutokana na kupigwa risasi na walinzi wa mgodi wa Mwadui ni kwamba kuna
makundi mbalimbali yaliyoachwa kusikilizwa na Kamati ya Ndugai na bila kuyataja
makundi hayo ripoti hiyo inakuwa haijakamilika na inakuwa na doa lisilofutika.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa gazeti hili umebaini kuwa
Kamati hiyo ilipata kigugumizi cha kukutana na wahanga waliopata ulemavu
kutokana na kushambuliwa kwa risasi za moto na walinzi wa Kampuni ya Zenity
Security inayolinda rasrimali za mgodi wa Mwadui pamoja na walinzi wa Kampuni
ya Elhilal Mining ambapo baada ya kulalamika sana wahanga hao waliahidiwa na
Kamati hiyo kwamba wangekutana na Wajumbe wa Kamati hiyo Mjini Dodoma kabla ya
kukabidhi Ripoti kwa Rais John Pombe Magufuli na sasa wanajiuliza! kwa kuwa
Kamati hiyo imekabidhi ripoti hiyo bila kuwasikiliza watapata wapi tena nafasi
ya kukutana ili waweze kueleza matatizo yao?
Katika hatua nyingine George na wenzake wamemuomba Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya uchunguzi wa Viongozi wa Jeshi la
Polisi waliokaa muda mrefu Mkoani Shinyanga maana kuna taarifa za kuwepo kwa
namna Fulani ya ushirikiano kati ya taasisi za Serikali na Makampuni
yanayofanya shughuli zake katika eneo la Mwadui.
“ kuna kesi nyingi za mauaji,kujeruhi kwa silaha za moto
zimekuwa zikizimwa muda mrefu kwa ushirikiano wa madaktari wa Hospitali ya
Serikali wakati wa uchunguzi wa majeruhi zikiwemo maiti baada ya mauaji
yanayotokana na walinzi wa mgodi wa Mwadui na Elhilal inayomilikiwa na
Phantom”.alisema George.
Ameyataja makundi hayo kama ifuatavyo.
Waliopigwa risasi na kupata ulemavu wa kudumu.
Katika kundi hili George anasema liko na watu wafuatao, yeye
mwenyewe George Joseph Bwisige (alipigwa risasi na kupelekea kukatwa mguu wa
kulia lakini hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa),Hamud Said , Marco
Ngussa (ambaye alipigwa risasi na kupasuliwa bandama),Nyalulu Sitta (alipigwa
risasi na kutobolewa jicho),
Kundi lingine ni la watu waliouawa kwa kupigwa risasi na Askari
wa mgodi.
Hawa ni Benard Edward maarufu (Mayo), Shilagi Masali mkazi wa
Masagala,Jishosha Daud, Hamad Shunda Mkazi wa Ikonongo ambaye hakuonekana
isipokuwa nguo zake pekee tu ndiyo zilizoonekana
Hawa ni kundi dogo tu ambao taarifa zao zimeweza kupatikana na
wengi wamepotelea katika mashimo yenye kina kirefu baad ya kukimbizwa
wakielekezwa huko kwa lengo la kuwaua na wanamuomba Rais Magufuli aweze
kuangalia utaratibu unaofaa ili kuwapatia kifut jasho waweze kukidhi mahitaji
ya kibinadamu maana wamefanyiwa ukatili usiowezakusahaulika maishani mwao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amekabidhiwa Ripoti Maalumu ya kuchunguza Biashara ya Madini ya Almasi na
Tanzanite nchini 7 Agosti 2017 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassim Majaliwa tukio lililofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Kabla ya kukabidhiwa Ripoti hizo kwa Rais Magufuli na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai alizipokea ripoti hizo kutoka kwa
Wenyeviti wa Kamati Maalumu alizoziunda ambazo zilijumuisha Wabunge wa Bunge la
Tanzania kutoka vyama mbalimbali vya Siasa.
Kamati hizo ziliongozwa na Dotto Biteko aliyeongoza Kamati ya
kuchunguza biashara ya Madini ya Tanzanite na Mussa Azzan Zungu Kamati ya
kuchunguza biashara za Madini ya Almas.
Kamati hizo ziliundwa wakati wa Mkutano wa Saba wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuchunguza mfumo bora wa
uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya Almas na
Tanzanite.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hizo, Rais Magufuli
amemtaka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwaita Wataalamu na
Taasisi zote zinazohusika na masuala ya madini kufanya maandalizi ya kubadili
Sheria zitakazosaidia Taifa kunufaika na rasilimali zake za madini.
“ Huu ndiyo wakati wa kubadilisha sheria zetu. Mhe, Waziri
Mkuu uwaite Wataalam wote wanaohusika na madini maandalizi haya yaanze haraka,”
amesema Dkt. Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amesisitiza suala la uzalendo kwa
Watanzania wote katika kusimamia rasilimali za nchi na kusema kuwa, ikiwa
watanzania wataweka mbele uzalendo Taifa litasimama na kwamba hatutochezewa na
wawekezaji tena na mikataba mibovu ambayo italiingizia Taif letu hasara.
Dkt. Magufuli amesema hivi sasa uchumi wa Tanzania unakua kwa
asilimia 7 hadi 7.1 na nchi ya nne nyuma ya nchi ya Ethiopia ambayo uchumi wake
unakua kwa asilimia 8.3 na kueleza kuwa, iwapo rasilimali hizo zingesimamiwa
vizuri taifa lingenufaika zaidi na kuwa na uchumi zaidi ya nchi ya India ambayo
haizalishi madini ya Tanzanite lakini imekuwa ni muuzaji mkubwa wa madini hayo.
“ Tutangulize maslahi ya nchi yetu mbele,nataka tufike
mahali tuanze upya,Mhe. Spika muendelee kutusaidia katika kusimamia rasilimali
zetu, amesema Dkt. Magufuli.”
Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
Wateule waliotajwa katika ripoti hiyo kukaa pembeni ili kupisha vyombo vya
Ulinzi na Usalama kufanya kazi yake vizuri.
Rais Magufuli amesema hayo yote yanafanyika ili kuh akikisha
kwamba watanzania wananufaika na rasilimali hizo na kueleza kuwa, bado
watanzania hawajanuifa vya kutosha na rasilimali za nchi ikilinganishwa na
rasilimali zilizopo.
Awali, akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti hizo, Waziri Mkuu
Majaliwa alisema kuwa, Kamati mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge zimefanya
kazi kubwa na hali hiyo inatokana nia ya dhati aliyoionyesha Rais Magufuli
kuhakikisha,rasilimali za madini zinakuwa na tija kwa Taifa.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Job Ndugai alisema kuwa, Bunge liko tayari kuzipitia na kuzifanyia
marekebisho Sheria zote ambazo hazilinufaishi Taifa na kueleza kuwa ipo haja ya
kulifanyia kazi suala la mifumo ya udhibiti wa rasilimali hizo.
Ndugai amewataka viongozi wa Serikali waliopewa dhamana ya
kusimamia shughuli za Umma kuguswa na umaskini wa Watanzania na hivyo kuzitaka
Bodi mbalimbali nchini kubadilika na kuona haja ya kuangalia na kufuatilia kwa
karibu maeneo wanayoyasimamia.
Akiwasilisha ripoti ya Madini ya Almasi Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mussa Azzan Zungu alisema soko la madini ya Almasi bado liko katika
kiwango duni japokuwa Almas yenye thamani ya juu inapatikana Tanzania pekee.
a
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Tanzanite Dotto
Biteko alieleza kuwa, asilimia 80 ya Tanzanite inatoroshwa nchini na asilimia
20 ya madini hayo ndiyo yanayoingia katika mfumo wa kodi nchini.
MWISHO.
Subscribe to:
Posts (Atom)