Boda boda Usagara hawana Leseni
Na Antony
Sollo Mwanza.
26june
2014
WAENDESHA Pikipiki wengi Usagara hawana leseni imefahamika,akizungumza
na waendesha bodaboda katika Mtaa wa Usagara eneo la Mizani Afisa wa Jeshi la
Polisi CPL Bakari Mwakipiko alibainisha kuwepo kwa waendesha bodaboda wengi
ambao hawana leseni ya udereva na pia wakiwa hawajui sheria za Usalama
barabarani.
Bakari alisema kuwa amesikitishwa na ukiukwaji wa sheria za
usalama barabarani unaofanywa na waendesha pikipiki hao na kusema kuwa hicho ni
chanzo kikubwa cha ongezeko la ajali nchini kwa kuwa vijana hao wanaponunua
pikipiki hizo tu huingia barabarani na kuanza kuendesha bila kupata mafunzo ya
aina yoyote jambo ambalo amekemea vikali.
Bakari amesema kuwa Serikali itawachukulia hatua kali wale
watakaoendelea kukaidi maelekezo ikiwemo kupata mafunzo ya uendeshaji wa vyombo
hivyo pamoja na leseni za kuendeshea.
“Nawaonya haya mambo ya uvunjaji wa sheria sasa yamefikia
mwisho,tumewaangalia muda mrefu maana mmekuwa mkifanya mambo yenu kama kwamba
serikali haipo,sheria inawataka muendeshe vyombo hivi mkiwa mmevaa kofia,lakini
pia kubeba abiria kufuatana na maelekezo ya mtengenezaji wa chombo” alisema Bakari.
Serikali imetambua kazi yenu kuwa ni ajira kwa mujibu wa
sheria nawashangaa mnapokiuka kanuni na taratibu zilizowekwa mnataka tuwafanye
nini?alihoji CPL Bakari.
Nawaomba muunde uongozi ili muweze kutambulika katika eneo
lenu kisheria,na muweze kusaidiwa na mifuko yenu mtakayokuwa mnachangishana ili
hata kama mmoja wenu atapata matatizo aweze kupata msaada.
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limeendelea kutoa elimu kwa
waendesha Pikipiki maarufu Bodaboda ili kupunguza ajari za barabarani huku
tafiti mbalimbali zikionyesha kuwa chanzo cha ajari nchini ni waendesha
pikipiki na waendesha baiskeli.
0 comments:
Post a Comment