Dk Kamani amwaga misaada jimbo la Busega
Na Antony Sollo Busega.
Julai 24.2014
Mbunge
wa jimbo la Busega ambaye pia ni WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi Dk Titus Kamani amemwaga mamilioni katika Jimbo la Busega
Mkoani Simiyu ikiwa niutekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi pamoja na
ahadi alizotoa wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa
2010.
Dk Kamani
amezindua miradi mbalimbali jimboni humo ambapo kati ya miradi hiyo ni mradi wa
ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri ya wailaya ya Busega utakaogharimu
shilingi milioni 500,000,000.
Akizungumza
na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamanyili Nassa jineri Dk
Kamani aliwashukuru wananchi nkwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Busega.
“Ndugu
zangu naomba kuwapongeza kwa mambo matatu,nawapongezeni sana kwa kunichagua
kuwa Mbunge wenu,pili kwa kujitokeza kwa wingi katika ziara ya Katibu Mkuu wa
Chama cha Mapinduzi pamoja na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
Jakaya Kikwete kwa ajili ya uzinduzi wa Mkoa wetu mpya wa Simiyu”.
Kuhusu
Makao Makuu ya Wilaya Dk Kamani alisema kuwa namshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa
kuichagua Wilaya ya Busega kuwa Makao Makuu ya Wilaya ambapo Kata ya Mwamanyili
lakini pia kwa uamzi wake wa kumalizia ziara yake Katika Wilaya ya Busega
ambapo ziara hiyo imezaa matunda mengi kwa kuelekeza miradi mbalimbali
inayoendelea hadi sasa.
Nawapongeza
pia kwa kuwa tayari kutoa maeneo kwa ujenzi wa nyumba za watumishi wa
halmashauri lakini pia mtafanya biashara kwa kuwa Makao makuu yako katika
maeneo yenu,hongereni sana.
Kuhusu
elimu Dk Kamani alisema kuwa,tangu aingie madarakani amesimamia ujenzi wa
Sekondari tatu ambapo amezitaja shule hizo kuwa ni Mwasamba,Mwamagigisi na
Kijirimi.
Dk Kamani
ameahidi kupeleka umeme wa jua katika ya Msingi Kishamapanda,na pia
aliwapongeza wananchi wa Nyang’hanga kwa uamzi wao wa kujitolea kujenga shule
na kuahidi kuchangia shilingi 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa choo na mabati
100.
Mwisho
![]() |
Dk Kamani akizungumza na wazee wa Kijiji cha Yitwimila muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kijiji hicho |
![]() |
Dk Kamani akikagua jengo la Ofisi ya Kijiji cha Yitwimila lililojengwa na wananchi |
![]() |
Dk Titus Kamani alipowasili kukagua mradi wa umeme huko Nyangili julai 25 2014 |
![]() |
Dk Kamani akiwa na mjumbe wa Mkutano wa Mkoa simiyu kabla ya kuhutubia mkutano wa wananchi |
![]() |
Dk Titus Kamani akipata taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji kabla ya kufungua mradi wa maji |
![]() |
Dk Titus Kamani akifurahia jambo baada ya kusikiliza kikundi cha ngoma wakati wa zira yake katika kata ya Nyangili Busega. |
![]() |
Dk Kamani akiangalia vifaa vinavyotumika kufunga umeme katika mradi wa REA unaotekelezwa jimboni Busega. |
![]() |
Dk Kamani akimsikiliza Katibu wa CCM Wilaya ya Busega baada ya kukagua mradi wa umeme vijijini REA jimboni Busega Picha na Antony Sollo Tanzania Daima |
![]() | |
Dr Kamani akiwa na viongozi mbalimbali katika jimbo la Busega akiwa na ziara ya kukagua nmiradi mbalimbali jimboni humo julai 24 2014. Picha zote na Antony Sollo wa Tanzania Daima. |
0 comments:
Post a Comment