August 08 2014.
Timu ya
Chitah FC yenye makao yake katika kijiji cha Ng’ombe Kata ya Igokelo,imeulalamikia
uongozi wa chama cha Mpira wa miguu Wilayani Misungwi MDFA kwa kile ilichodai
kufanyiwa utapeli wakati wa kushiriki ligi
daraja la nne iliyomalizika hivi karibuni Wilayani humo.
Akizungumza
na Tanzania Daima Mwenyekiti wa Chitah FC Emanuel Saba kalezu alisema,timu hiyo
ilionekana kuwa na wachezaji bora,wenye
mvuto na wenye kujituma katika mchezo wa mpira wa miguu Wilayani Misungwi.
Emanuel
alifafanua kuwa,baada ya timu hiyo kuwa kivutio kwao,Viongozi wa Wilaya ya Misungwi waliwashawishi
wachezaji hao kushiriki ligi hiyo kwa hila ili kuwaingiza katika mzunguko wa
ligi daraja la nne ngazi ya Wilaya hiyo huku wakijua fika kwamba timu hiyo
haikuwa na leseni ya kushiriki michuano hiyo.
Mwenyekiti
huyo aliwataja viongozi waliotumia ujanja ujanja huo kuitapeli timu hiyo kuwa
ni Hassan Mwakami Katibu wa MDFA Wilaya
ya Misungwi na Msaidizi wake Sylivester Nyanda.
Imedaiwa
kuwa timu hiyo ilikubali kushiriki
ligi hiyo lakini wachezaji hao wamebaini kuwa kulikuwa
na njama iliyokuwa imeandaliwa na Viongozi wa MDFA na hawakutegemea kama timu
hiyo ingeweza kufikia hapo ilipofika kwa kunyakua ubingwa wa Ligi ngazi ya
Wilaya ya Misungwi kwa mwaka 2014.
Baada ya
ushindi huo,Viongozi wa MDFA Wilaya ya Misungwi wanadaiwa kufanya mchakato wa kubadilisha
ushindi wa Chitah FC kuwapa
ushindi huo kwa timu ya Halmashauli ya Wilaya ya Misungwi Winners FC,ambayo hata hivyo timu hiyo ilishika nafasi ya 4
kati ya timu 6 zilizoshiriki ligi hiyo
ikiwa na point 7.
Huku
Chitah FC wakimaliza ligi hiyo wakiwa
point 11.
Timu
zilizoshiriki michuano hiyo ni Chitah FC
imefunga magoli 7 imefungwa magoli 2 Point 11 ,
Stand FC
Misungwi imefunga magoli 7 kufungwa magoli 3 Point 8 ,
Brek FC
ya Kijiji cha Nguge imefunga magoli 7
imefungwa magoli 4 Pointi 7 ,
Misungwi
Winners inayomilikiwa na Halmashauri ya
Wilaya ya Misungwi, imefunga magoli 11 imefungwa magoli 10 Point 7
Kwiki
Sport Club ya Kijiji cha Wanzamiso imefunga magoli 4 imefungwa magoli 5 ina Point
7.
Vijana FC
ya Kijiji cha Mapilinga imefunga magoli 3 imefungwa magoli 19 ina Point 0
Tanzania
Daima ilipata nakala ya barua ya Chita FC ya tarehe 04 August 2014 kwenda Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza MZDFA iliyokuwa
ikipinga ushiriki wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika ligi ya
Mabingwa kwa kuwa haikuwa na sifa ya kushiriki ligi hiyo.
Wachezaji
wa Chita FC wamekiomba Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza MZDFA kusaidia kusimamia
haki na wahusika wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuwa vitendo hivyo
vinazorotesha soka nchini.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment