Na Antony Sollo Geita.
August 08.2014.
MWANDISHI wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Wilayani Geita
Valence Robart,amenusurika kupigo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Wilaya
ya Geita,OCD Busee Bwire,muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo imefahamika.
Robart alifika kituoni hapo akifuatilia maendeleo ya kesi
aliyoifungua kituoni hapo julai 23 mwaka huu baada ya kuibiwa pikipiki yake
aina ya SUNLG yenye namba za usajili T305 BWV ambayo iliibiwa na watu
wasiojulikana.
Tukio la kutishiwa kupigwa na OCD Bwire lilitokea Aug 5 mwaka huu
majira ya saa nane na nusu mchana muda mfupi baada ya Robert kuwasili
kituoni hapo kwa lengo la kuonana na mpelelezi wa kesi yake GE/RB/4617/2014
ambayo ilifunguliwa kituoni hapo.
Mara baada ya kufika kituoni hapo Robert alianza kuzungumza na Mkuu
wa Kituo cha Polisi Geita Enock Rayi hapo mapokezi CRO, ghafla alitokea OCD
Bwire ambaye kwa wakati huo alikuwa ofisini kwake.
“Unashida gani kituoni hapa?umefuata nini?”OCD Bwire aling’aka.
Robert alijibu kwa upole nilichofuata hapa ni huduma,yaani
nimekuja kufuatilia maendeleo ya kesi yangu kufuatia kuibiwa kwa Pikipiki yangu.
Imedaiwa kuwa OCD Bwire alimtaka Mwandishi huyo kuondoka mara moja
eneo la kituo hicho kabla ya kuagiza awekwe Mahabusu kitendo ambacho
kilionyesha udhalilishaji kwa raia badala ya kutekeleza majukumu ya ulinzi wa raia
kama lilivyo lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa Jeshi la Polisi .
“Ondoka hapa mara moja kabla sijakuweka sero,nitolee sura yako
hapa mara moja’’alisikika OCD Bwire akimfokea Mwandishi huyo ambaye baada ya
vitisho hivyo Robert aliondoka Kituoni hapo.
Tanzania Daima lilifuatilia sakata hilo na kubaini kuwa kuna
msuguano mkali baina ya Mwandishi na OCD Bwire kwa kuwa mara kadhaa aliwahi
kuripoti matukio mbalimbali yanayofanywa na Bwire. matukio ambayo yamepelekea
kulidhalilisha jeshi hilo.
Imebainika kuwa matukio yaliyomuudhi Bwire ni kuripotiwa kwa tukio
la kuangusha gari la Jeshi hilo alilokuwa akiliendesha yeye wakati likitokea
katika kituo kidogo cha Polisi nyarugusu
likiwa na watuhumiwa ambao walitoroka baada ya ajali hiyo huku kazi hiyo
akihodhi mamlaka ya uendeshawaji wa gari hilo.
Tukio lingine ni lile la kumshambulia Mkewe Taus Mashaka na
kumuuma mdomo hali ambayo imepelekea mwanamke huyo ambaye pia ni askari Polisi kitengo
cha Usalama Barabarani kutimkia nyumbani kwao singida.
Tanzania Daima lilipomtafuta OCD Bwire kuzungumzia madai ya
kumtishia na kutaka kupiga Mwandishi Bwire alijibu kwa mkato “mimi sijui”
Robert amemuomba Mkuu wa polisi nchini IGP Ernest Mangu
kumwajibisha Askari huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni amefanya kitendo
kinachokinzana na masuala ya Haki za Binadamu ikiwemo ukatili wa Kijinsia kwa
kumpiga mkewe huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kimnyume na Maadili
ya Jeshi hilo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment