Sunday, April 13, 2014

TAARIFA YA SNDF KUHUSU KAMPENI YA ASASI ZA KIRAIA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KANDA YA ZIWA- MKOANI SHINYANGA 2014.

SHINYANGA NGUVUKAZI DEVELOPMENT FOUNDATION (SNDF)
              P. O. BOX 1288, MHUNZE-KISHAPU-SHINYANGA (TZ)
              Mobile:+255 762 117 117 / +255 785 118  118
              Email::sndfoundation@ymail.com

TAARIFA  YA  SNDF  KUHUSU  KAMPENI  YA  ASASI ZA  KIRAIA  KUSAMBAZA  UELEWA  WA RASIMU  YA PILI YA  KATIBA  YA JAMHURI  YA  MUUNGANO  WA  TANZANIA  KANDA  YA ZIWA- MKOANI  SHINYANGA  2014.

Utangulizi
SNDF ni Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiriwa kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002 ambapo shirika hili lilisajiliwa Sept 20 .2011.
Shirika hili linafanya kazi kwa kushirikiana na Kituo cha sheria na haki za binadamu katika masuala yanayohusu utetezi wa haki za binadamu.
Makao Makuu ya Shirika hili yapo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga

ASASI  YA  NSDF   Inapenda  kutoa  Taarifa  juu ya  mpango  wa  AZAKI  kuandaa  kampeni  ya  kusambaza uelewa  wa Rasimu ya pili  ya  Katiba  ya  Jamhuri   ya  muungano  wa Tanzania.

Mpango  huu  ni  mpango  ambao  Umekuwa  ni  Kipimo  na Dira  kubwa na  ni  mtihani  ulioweza  kuwapima  Watanzania  na kuelewa .  kama Iwapo  walikuwa  na  Uelewa  kiasi  gani  kuhusu  katiba  ya jamhuri  ya  Muungano  wa Tanzania   na  uhusiano  wa  zoezi la  sasa  kuhusu   Rasimu  ya  pili  ya Katiba  ambapo  zoezi hili Iimezua  Zogo  na Mjadala  Mkubwa  Bungeni  Dodoma.

Awali  ya  yote  napenda  kuitambua  kazi  kubwa  iliyo  fanywa kwa ushirikiano  wa LHRC na Asasi 14  juu  ya  kuandaa   mpango   huu ambao  ni mzuri  ili  kuweza  kupata  Dira juu ya  uelewa  wa rasimu ya Katiba kwa  Watanzania

Kuhusu  historia  kubwa   katika  Nchi  kwa  kuwa zoezi  la  kuandika   katiba  ya  Nchi  Chini  ya Mamlaka  yao   ndiyo  linafanyika  kwa mara   ya  kwanza   tangu  Nchi  yetu  ipate  Uhuru   tarehe  9.Dec. 1961.

Lakini  pia  napenda  kutambua  kazi  zilizofanyika  awali  ikiwemo  uteuzi  wa Tume  ya  mabadiliko  ya  katiba. Tume  ambayo  iliteuliwa  na Mh.  Rais  wa Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania   Jakaya   Mrisho  Kikwete  na  kumpa  Uenyekiti  wa Tume  hiyo  Mh.  Jaji  Mstaafu  Joseph   Sinda  Warioba.

Tume  hii  Imefanya  Kazi  yake  kwa  Weledi   mkubwa,  imeweza  kuisimamia   vyema  sheria  ya Mabadiliko   ya  katiba  Namba 83,  ya  Mwaka  2011  na  kutimiza vizuri   wajibu   wake   katika  kukusanya  Maoni ya Wananchi, kufanya utafiti, kuratibu  na  kuandaa  Rasimu ya kwanza  na ya pili  ya katiba. 

Tumeshuhudia  jinsi  tume ya  Mh. Jaji, Joseph, Warioba  ilivyofanya kazi, nzuri  katika  kutetea  Maoni  na Mawazo  yaliyotolewa   na Wananchi  maoni ambayo  ndiyo msingi  mkuu  wa  utungaji wa katiba ya kidemokrasia, inayoshirikisha wananchi wote kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.

Mchakato wa kuandika katiba mpya sio jambo dogo la kubezwa, kuingiliwa na taasisi yoyote ile kwa lengo la kutetea maslahi binafsi ya kundi hilo, bali ni ushirikishwaji wa wananchi na kuweka mbele matakwa yao na kuyazingatia, jambo ambalo litawafanya waheshimu masharti yaliyomo katika katiba hiyo.

Kwa dhati kabisa, nawapongeza Wabunge wa Bunge Maalum la katiba ambao wako mjini, Dodoma wakiendelea na uchambuzi wa Rasimu ya pili ya katiba ambapo na pia naomba watambue kuwa kuteuliwa kwao kuwakilisha makundi mbalimbali kutaleta heshima tu iwapo wataweka mbele masilahi ya watanzania badala ya kuweka mbele itikadi za vyama vyao, ubinafsi na watambue kwamba,mchakato  wa  kukusanya  Maoni ya  Wananchi ,  kuhakiki  kupitia  Mabaraza  ya  katiba  ulifanyika  kwa uwazi  na  kwamba   Rasimu  ya pili  imebeba  utashi  wa Wananchi, hivyo  inahitajika,  hekima,  busara  zaidi  wakati  wa mjadala  na kupitisha  Rasimu  ya pili  ya  katiba.

Nchi  yetu  imepitia   hatua  mbalimbali  tangu Uhuru   na  baada  ya  Kuziunganisha  Nchi, Mbili  yaani  Tanganyika na Zanzibar, hivyo  mapendekezo  yaliyomo  kwenye  rasimu  ya  pili  ya  katiba  yatakuwa  na   uhalali na heshima  kubwa  iwapo tu  mawazo   ya  Wananchi yatapewa nafasi  kuliko   kuendekeza  ushawishi  wa  kiitikadi wa vyama vya siasa  na ubinafsi.
Baada  ya  Bunge  Maalum  la  katiba  kupitisha   rasimu  hatua  inayofuata  ni Wananchi  Kuridhia Mapendekezo yaliyotolewa na Bunge  Maalum  kwa   njia  ya  kupiga   kura.
Lakini  pia kuna  uhitaji  mkubwa  wa   kutoa  Elimu  kwa  Wananchi ili  waje  kufanya  kazi  hii  kwa umakini mkubwa,huku wakielewa vyema haki na wajibu wao katika ushiriki wao ili tuweze kupata katiba nzuri itakayotuongoza kwa zaidi ya maika 50 ijayo.



MANUFAA  YA KAMPENI YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI YA KATIBA 2014

Mpango wa LHRC na Asasi 14 uliozinduliwa kanda ya magharibi tarehe 22 March 2014 huko Kigoma umeleta manufaa makubwa kwa Watanzania kwani kabla ya kampeni na baada ya kampeni hii  viashiria vinaonyesha, jinsi mpango huu ulivyowavutia Watanzania na kuwafanya wawe na hamu, ya kuelewa Rasimu ya pili ya katiba na mwendelezo wa hatua ya mwisho ili kuona, iwapo Bunge litakuwa limetimiza matakwa yao kwa kuheshimu mawazo na mapendekezo yao yaliyomo katika, Rasimu ya pili ya katiba.

PONGEZI:
Napenda kuwapongeza Viongozi wa Mkoa wa Shinyanga na Wilaya zote kwa ushirikiano mkubwa toka kwao pamoja na watendaji wa Serikali, kwa kusimamia na  kuhakikisha kampeni hii inawafikia Watanzania Mkoani Shinyanga bila vikwazo, huu ndiyo uzalendo unaopaswa kuigwa katika maeneo mbalimbali nchi ili kutoa nafasi kwa Watanzania kuweza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Utungaji wa Katiba Mpya jambo ambalo ni la kihistoria katika nchi yetu.

Vilevile Pongezi hizi ziwaendee wanahabari wa Vyombo mbalimbali nchini kwa  mchango wao mkubwa sana katika kuhabarisha na kuelimisha wananchi juu ya kampeni hii mkoani Shinyanga na sehemu mbalimbali ,nina imani kuwa,zoezi hili likiendelea hivi nchi nzima, uelewa wa Watanzania utaongezeka maradufu na zoezi la upigaji kura kwa hatua ya mwisho baada ya kumalizika kwa mijadala ya  Bunge maalumu kumaliza kazi yake wananchi watapiga kura huku wakielewa ni nini wajibu wao katika hatua ya Mwisho.   

Taarifa hii imeandaliwa na:
Antony Johnson Sollo,
Mkurugenzi wa,
Shinyanga NguvuKazi Development Foundation SNDF.
S.L.P 1288,
Kishapu,
Shinyanga.
www.sndffoundation.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment