Dk. Kamani, adaiwa kugawa fedha kwa Wajumbe
wa CCM
Na Antony sollo
Busega .
WAZIRI wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega Mkoani
Simiyu, Dk. Titus Kamani, anadaiwa kugawa fedha kama ‘njugu’ kwa baadhi ya
wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo ili
wamuunge mkono katika harakati za kisiasa..
Akizungumza na Tanzania Daima Madirisha alisema kuwa Dk. Kamani alikutana na wajumbe hao kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari Mosi hadi Januari 3 mwaka huu katika hoteli hiyo, ambapo inadaiwa licha ya kuwagharimikia chakula na vinywaji alimpatia kila mjumbe Sh 30,000/=
“Hawa wajumbe ni wale wanaotoka kwenye matawi ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Busega. Kila tawi waliitwa wajumbe watano ambapo Jimbo la Busega lina vijiji 59 ,Waziri Kamani alianza kukutana nao tarehe moja hadi tarehe 3 kwenye hoteli yake ile ya Stop Over ya hapa Lamadi” alisema madirisha.
Mmmoja wa makada wa CCM aliyejitambulisha kwa jina Buzuka aliliambia gazeti hili kuwa Kamani anaendekeza siasa za chuki na fitna dhidi ya watu wanaoonekana kupingana na yeye katika harakati zake za kisiasa huku akishindwa kutekeleza ahadi zake nyingi alizowaahidi wananchi katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Buzuka alisema kuwa,moja ya sababu zilizopelekea wananchi wa Lamadi kupigwa mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la polisi ni kutokana nashinikizo la Dk Kamani kutaka wagombea wote wa CCM wapite bila kupingwa huku ikitumika njia ya kuenguliwa kwa wapinzani na mpaka sasa kuna magunia 50 ya msaada hapa Lamadi yameshindwa kushushwa na kugawiwa kwa walengwa kutokana na kutotambuliwa kwa wenyeviti wa mitaa waliopitishwa kwa nguvu na Dk Kamani,” alisema Buzuka.
Tanzania Daima lilipohojiana na Dk Kamani kuhusu tuhuma hizo alikiri kualika watu na kuwakirimu,lakini alisema kuwa yeye ni kiongozi aliyeko madarakani,na anayo haki ya kukutana na wananchi waliomchagua kuwa kiongozi wao wakati wowote na hazuiliwi na mtu yeyote kufanya hivyo .
“ Ni kweli niliwaalika watu wa makundi mbalimbali,mimi ni kiongozi wao , na si mara yangu ya kwanza kuktana na wananchi,nilishajiwekea utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali katika jamii kama vile walemavu,wazee,vijana na wasiojiweza niliwapatia nauli kama ulivyoelezwa maana hawa watu wanatoka sehemu tofautitofauti hivyo ni lazima ukiwa na upendo uonyeshe fadhila ” alisema Kamani.
Kuhusu kushindwa kugawiwa kwa magunia 50 ya Mahindi,Dk Kamani aliangua kicheko na baada ya kicheko hicho alisema “jamani siasa za nchi hii!! Mimi niko Dar es salaam nawezaje kuzuia mahindi yasigawiwe kwa wananchi?”alihoji Dk Kamani.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment