Friday, January 30, 2015



Chegeni:  Serikali itenganishe wizara 
Na Antony Sollo Dodoma
jan 30 2015

MJUMBE WA Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Buesga Dk. Raphael Chegeni ameishauri Serikali ijayo kutenganisha Wizara ya Nishati na Madini, ili kuleta ufanisi na uwajibikaji thabiti na kuondoa matatizo ya kufukuzwa kazi mara kwa mara kwa Mawaziri wanaoongoza wizara hiyo.

Akizungumza naTanzania Daima Dk Chegeni alisema kuwa, Wizara  ya Nishati na Madini imekuwa mwiba kwa Mawaziri wanaokabidhiwa madaraka ya kuiongoza kutokana na ubovu wa mfumo wake, hivyo,Serikali inapaswa kuitenganisha ili Nishati ijitegemee zikiwemo na Wizara zingine zenye mwingiliano kama huo. 

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Dk. Raphael Chegeni, alibezaa mabadiriko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete na kusema kuwa hii ni aibu kubwa kwa Serikali kwa kuweka  Mawaziri ambao hawakidhi na wasiokuwa waaminifu jambo lililopelekea kufukuzwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali.

Aliwataja Mawaziri walioondolewa kwa kashfa mbalimbali ikiwemo ya sasa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow kuwa ni Profesa Sospeter Muhongo, William Ngeleja, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.

“Wizara hii inamatatizo makubwa sana ya kimfumo, Kinachotakiwa sasa  Rais ajaye anapaswa kuleta mabadiliko katika Wizara zilizo nz mwingiliano ili kuzitenganisha, vinginevy Mawaziri wataendelea kuwajibishwa hata kwa makosa yasiyowalenga moaja kwa moja”.

“Unapozungumzia rasilimali ya Madini hapa utakutana na wawekezaji  wakubwa na wadogo wenye fedha zao. Vile vile kwenye rasilimali ya Nishati utakutana na wawekezaji wakubwa na wadogo katika biashara ya mafuta na gesi, hivyo uwajibikaji unakuwa na mushkeli kidogo,” alisema Dk. Chegeni.

Kuhusu Waziri mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Dk. Chegeni alisema kazi aliyopewa kiongozi huyo ni kubwa na nzito ikilinganishwa na muda mfupi uliobaki kabla haujafanyika Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba mwaka huu.

Dk Chegeni alimshauri Simbachawene kuacha siasa katika utekelezaji wa majukumu yake, bali ajikite kupeleka huduma za umeme vijijini ikiwa ni pamoja na Jimbo la Busega ambaolo (Dk. Chegeni) akiwa Mbunge wa Jimbo la Busega alipigania kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana mpaka Vijijini .

“Akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu ujao Dk Chegeni  alisema kuwa, muda uliobaki huu mfupi sana hivyo akamuomba Waziri wa Nishati George Simbachawene akaze buti maana Watanzania wanamtazama sasa,” 

Dk Raphael Chegeni amewaomba Watanzania kuombea Nchi isiingie katika machafuko kufuatia Masuala mawili makubwa yaliyo mbele yetu ambapo aliyataja masuala hayo kuwa na kura ya Maoni katika Katiba Pendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.

MWISHO:
Mobile:  0785 118 118 / 0762 117 117 /0784 114 114

0 comments:

Post a Comment