Na Mwandishi wetu Mwanza.
Sababu ya kufukuzwa kwa
wanahabari katika kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Misungwi,imewekwa hadharani
imebainika kuwa kuna siri kubwa nyuma ya tukio hilo.
Kufukuzwa kwa waandishi wa habari
Antony Sollo Valence Robert na Twallad Salum waliokuwa wamehudhuria kikao cha
Baraza la Madiwani kilichofanyika Jumamosi 2 mwaka huu,kimetokana na Kaimu Afisa
Habari Thomas Lutego kutumwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Nathan Mshana ili
kuficha maovu yanayofanywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Imedaiwa kuwa Lutego na
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nathan Mshana wamekuwa na mgogoro wa muda mrefu
na Mwandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Twallad Salum baada ya Mwandishi
huyo kufichua maovu yanayofanywa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Misungwi.
Lutego amekuwa jeuri, na
amekuwa akichagua waandishi wa habari watakaofika katika Halmashauri ya Wilaya
ya Misungwi kwa maelekezo toka kwa Mkurugenzi Mshana ili kuripoti wanachotaka
wao,na si hali halisi ya matukio yanayofanyika katika halmashauri hiyo.
“ unajua halmashauri yetu
imekuwa na matukio mengi ya kifisadi,sasa wakiruhusu wanahabari wengine wafike
kuyaripoti siri zinaweza kuvuja matokeo
yake inaweza kuleta matatizo katika utendaji na kuathili kundi linalolengwa
kufichiwa maovu yake.”kilisema chanzo cha taarifa hizi”
Moja ya madudu yanayokingiwa
kifua na kufichwa ili yasijulikane ni tukio la wizi wa mafuta ulifanywa na
Dereva George Sanga ambaye ni mtoto wa
Diwani wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi Beatrice Kaburule ambaye ni
mjumbe wa kamati ya Ukimwi baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi.
Imedaiwa kuwa sakata la wizi
wa mafuta lita 290 uliofanywa na Sanga,umepelekea kumkandamiza Dereva Justine
Malimi ambaye imedaiwa kuwa wakati wizi huo unafanywa alikuwa mgonjwa lakini
hadi sasa ametolewa kafara kwa ajili ya kumlinda Sanga ambaye ni mtoto wa
Diwani huyo ili aendelee na kazi katika halmashauri hiyo.
“Sakata hili kwa sasa lina limepewa
sura ya kisiasa ili kuuficha ukweli wa mambo yanayoendeshwa hapa Misungwi,
Malimi amehusishwa na wizi wa mafuta lakini kila kitu kiko wazi mhusika wa wizi
wa mafuta lita 290 tunamfahamu,ni George Sanga”alisema Dereva mmoja wa Halmashauri
hiyo na ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usalama wa kibarua chake.
Taarifa zimeendelea kumiminika
kuwa Beatrice amejinufaisha kwa kuweka mradi hewa wa kuku hapo kwake na
imedaiwa kuwa alichota fedha za mradi na kuweka kwenye mradi wake ambapo kuna
banda la kuku lakini hakuna hata kuku mmoja kama inavyodaiwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Nathan
Mshana kutifuana na Mwandishi wa gazeti Mwananchi Twaladi ni baada ya
kuripotiwa kwa mradi hewa wa kuku 60 wenye thamani ya shilingi mil 10,000,000 ambapo Mshana alidanganya
kuwepo kwa mradi huo hewa ambapo wanahabari walifika na kukuta hakuna kuku hata
mmoja.
Baada ya Twallad kuripoti
ukweli huo ikawa ndiyo chanzo cha
mgogoro huo kati yake na kuingiliwa na Kaimu Afisa habari huyo,ambapo hadi sasa
haaliki waandishi wa maeneo ya Misungwi kwa kuwa wanajua siri nyingi
zainazotendeka katika Halmashauri hiyo.
Lingine kubwa kabisa ni
kutafunwa kwa fedha za ujenzi wa jengo la utawala katika Halmashauri hiyo kiasi
cha shilingi Mil 900.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi aliomba fedha kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
Utawala,fedha hizo zilikuja kwa awamu ambapo mwaka 2007 /2011 waliletewa
shilingi mil 600,000,000 ambazo walizitumia kwa shughuli nyingine.
Kaimu Afisa habari aliwaambia
waandishi hao kuwa hawaruhusiwi kuingia katika kikao cha Halmashauri hiyo kwa
kuwa si wahusika.
Imeelezwa kuwa waandishi hao
waliwaona viongozi mbalimbali wakimwemo Mbunge wa Jimbo la Misungwi Charles
Kitwanga,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Khalid Mbitiyaza n Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi ili waingilie kati mgogoro huo ambapo Mbitiyaza aliahidi
kulifuatilia suala hili.
Mpaka sasa taarifa
zilizopatikana kutoka chanzo cha habari hizi ni kwamba kutakuwa na kikao cha
dharula ili kuzungumza na Mkurugenzi pamoja na baadhi ya wahusika ili kulitafutia
ufumbuzi suala hili.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment